Thursday, 1 August 2013

Waliofanyisha mtoto ngono na mbwa washindwa rufaa waenda jela miaka 55.

MAHAKAMA ya Rufaa imetupilia mbali maombi ya rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, iliyowatia hatiani Shija Madata na wenzake wawili kutumikia kifungo cha miaka 55 jela baada ya kumfanyisha ngono mtoto na mbwa.
Rufaa hiyo ilitupiliwa mbali na jopo la majaji watatu; Natharia Kimaro, Ibrahimu Juma wakiongozwa na Jaji Januari Msofe, wakisema hoja za warufani hazikuwa na mashiko ya kubatilisha hukumu ya awali.
Akisoma hukumu hiyo jana kwa niaba ya jopo hilo, Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Bampikya Willibard, alisema baada ya majaji kupitia hoja za warufani walibaini hazina mashiko kulingana na kosa walilotenda.
Alisema kuwa waomba rufaa walitenda kosa baya. Kwamba mbali na kumshushia hadhi mwathirika wa tukio hilo, kulikuwa na mazingira ya kumsababishia magonjwa.
Alifafanua kuwa waliamuliwa kulipa kila mmoja fidia ya sh 200,000 na wataendelea kutumikia kifungo jela kama ilivyoamuliwa na mahakama ya mkoa.
Shija ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 18, kwa pamoja na wenzake walipatikana na hatia katika kesi ya kumlazimisha mtoto wa miaka 13 kufanya ngono na mbwa.
Mbali na Shija, warufani wengine ni Job Mlama, ambaye wakati huo alikuwa na miaka 30 na Anicet Edward, aliyekuwa na miaka 30, ambao walihukumiwa kifungo cha miaka 40 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia katika kesi hiyo.
Warufani walihukumiwa na Hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Gadiel Mariki, baada ya  kusikiliza mwenendo mzima wa kesi na kuwaona walikuwa na hatia kutokana na shitaka lililokuwa likiwakabili.
Kwamba kitendo walichokifanya kilikuwa cha kinyama na hakikustahili kuvumiliwa kwenye jamii iliyostaarabika kama Tanzania, hivyo akatoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine.
Shija anatumikia kifungo cha miaka 15 jela kwa kosa la kumrubuni mtoto na kumpeleka kwenye kambi ya madini ya Barrick kwa nia ya kumfanyisha ngono na mbwa.
Hakimu Mariki katika hukumu hiyo alisema katika kosa la pili watuhumiwa Shija, Job  na Anicet watatumikia kifungo cha miaka 20 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kumshawishi mtoto kukaa maeneo ya kambini na kumfanyisha ngono na mbwa.
Kwamba wote watatu watatumikia jela miaka 20 mingine kwa kosa la kumlazimisha kwa nguvu mtoto kufanya ngono na mbwa.
Mbali na adhabu hiyo kwa washtakiwa, Hakimu Mariki aliagiza wamiliki wa mgodi wa Barrick kumkabidhi mbwa huyo mikononi mwa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza ili amilikiwe na serikali.
Hata hivyo alisema kuwa watuhumiwa hao watazitumikia adhabu hizo kwa pamoja, hivyo watakaa jela miaka 20 kila mmoja na kusisitiza kuwa kama hawakuridhishwa na uamuzi wa mahakama hiyo wana haki ya kukataa rufaa.
Wakili Mfawidhi wa Serikali, Edwin Kakoraki, wakati huo, aliiambia mahakama kuwa  tukio hilo lilifanyiika Machi 21, 2008, ambapo watuhumiwa hao walikuwa kwenye kambi ya utafiti wa madini ya Barrick wilayani Sengerema.
Kwamba walimlazimisha mlalamikaji ambaye alikuwa mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Sota kufanya ngono na mbwa, ambapo siku ya tukio mlalamikaji alikwenda kwenye kambi hiyo akiwa na Shija ambaye ni rafiki yake baada ya kumfuata nyumbani kwao saa 1:00 usiku na kumuomba amsindikize kwa rafiki yake wa kiume, aliyekuwa mshitakiwa namba moja Job Mlama.
Mahakama ilielezwa kuwa Shija na mlalamikaji walipofika kwa Job, walipewa chakula na kisha maji ya kuoga, baadaye Shija alijilaza kitandani kwa Job na ilipofika saa 4:00, Shija na Job walimwambia mlalamikaji waende kwenye chumba kingine wakazunguke kisha watarudi.
Ilidaiwa  kuwa mlalamikaji alikubaliana na kauli ya rafiki yake, hivyo kuondoka wote watatu na kuelekea kwenye nyumba ambacho Shija na Job walikuwa wakimpeleka mbwa na walipofika kwenye banda la mbwa walimkuta Anicet ambaye ni mwangalizi wa mbwa.
Ilidaiwa kuwa watuhumiwa wote watatu walishirikiana kumvua mlalamikaji nguo zote na kumsukumia kwa mbwa dume mwenye rangi nyeusi na Anicet kumuonyesha ishara mbwa huyo ambaye alianza kumwingilia mlalamikaji.
Kwamba wakati mbwa huyo ikimwingilia kinyume cha maumbile, mlalamikaji alikuwa akipiga kelele kuomba msaada lakini washitakiwa wote watatu walikuwa wakicheka na kushangilia.
chanzo:daima

No comments:

Post a Comment