Wednesday, 18 September 2013

Diamond awatosa wasanii wa Bongo

MSANII wa muziki wa bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond Platinum’, amesema hatakubali tena kufanya kazi na wasanii wa Bongo ili kuepusha malalamiko kuwa amewaibia mashairi yao.
Kauli hiyo ya Diamond, imekuja baada ya hivi karibuni kudaiwa kuwa ameiba ‘beat’ ya wimbo wa Dyna pamoja na baadhi ya mashairi ya Baba Levo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Diamond alisema wasanii wengi wa Bongo hawana uelewa na ndio maana hawaendelei, hivyo hatorudia tena kushirikiana nao katika kazi zake.
“Unajua Bongo tuna wivu wa kijinga sana, ukiona mwenzako kaendelea tu unamtafutia kila namna ili aonekane mbaya, Dyna ana wimbo wake lakini haufanani kabisa na huu na kama ni suala la ‘beat’, kazi hii nimefanya Afrika Kusini zitafanana vipi?” Alihoji Diamond.
Wimbo ambao wasanii hao wanalalamika kuibiwa na Diamond, unaitwa ‘My Number One’ ambao unafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na runinga.
Diamond ni msanii anayefanya vizuri hivi sasa, akitamba na kazi zake kama, ‘Kesho’, ‘Kizai zai’, ‘Nataka kulewa’, ‘Nimpende Nani’, ‘Moyo Wangu’, ‘Mbagala’ na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri sokoni.
chanzo:daima

No comments:

Post a Comment