Wednesday 16 October 2013

Ajinyonga kwa madai ya kuchoshwa na ugomvi wa mara kwa mara na mkewe.

MKAZI wa Mchikichini Mafuriko, Saidi James, amekufa kwa kujinyonga kwa madai ya kuchoshwa na ugomvi wa mara kwa mara na mkewe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi, saa tatu usiku ambapo mwanaume huyo alijinyonga kwa kutumia mtandio wa mkewe.
Kwa mujibu wa Minangi sababu za kujinyonga inasadikiwa kuwa ni ugomvi wa mara kwa mara kati yake na mkewe, Mwanahamisi Omary (23).
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana

No comments:

Post a Comment