Friday 11 October 2013

Diamond atambia ‘movie’ yake na Wema

MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nassib Abdul ‘Diamond Platinum’, amesema kati ya filamu za Tanzania ambazo zitakuwa gumzo ni pamoja na aliyocheza na msanii, Wema Sepetu, inayojulikana kwa jina la ‘Temptation’.
Alisema filamu za Tanzania ni bora, lakini ana uhakika kazi hiyo itakuja kufunika soko kutokana na ubunifu waliotumia kuwateka wapenzi wao.
Diamond aliandika katika ukurasa wake wa ‘instagram’ kwamba kuna baadhi ya vipande vya filamu hiyo wamevicheza wakiwa China na kwamba, wana uhakika kazi hiyo itakuja kufanya vizuri katika soko kutokana na mazingira ambayo wameyatumia.
“Mengi yalisemwa hadi wengine kudiriki kumtukana Penny, lakini ukweli ni kwamba, hii ni ‘movie’ mpya kabisa iliyochezwa na mimi nikiwa na Wema na hakuna kingine kinachoendelea, hapa ni kazi tu,” aliandika Diamond kupitia ukurasa huo.
Diamond na Wema walikuwa na uhusiano wa kimapenzi, ambako Diamond alikiri ameachana na msanii huyo na badala yake akatangaza kuwa na uhusiano na mtangazaji wa DTV, Penny Mungilwa.
chanzo:daima

No comments:

Post a Comment