Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kupitia Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John Mnyika, kimesema kauli inayoenezwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye (pichani), kuwa Chadema kimeshindwa kusimamia katiba yake kwa kutofanya uchaguzi wa ndani kwa zaidi ya miaka kumi hayana ukweli wowote.
Mnyika kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari alisema Chadema tangu kuanzishwa kwake kimekuwa kikiheshimu katiba yake kwa kufanya chaguzi zake kwa mujibu wa katiba, kanuni, maadili, itifaki ya chama.
“Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita alichokizungumza Nape, Chadema kimefanya chaguzi mara mbili kila baada ya miaka mitano kama katiba na kanuni zinavyohitaji,”alisema Mnyika.
Alisema Chadema kimefanya uchaguzi mkuu wa ndani mwaka 2004 na kikafanya uchaguzi mkuu mwingine mwaka 2009 mara baada ya kipindi cha miaka mitano ambayo ni muda wa kawaida wa uongozi.
chanzo:nipashe
No comments:
Post a Comment