Monday 31 March 2014

Wolper akana kuwatosa wazazi

STAA wa filamu za bongo, Jacqueline Wolper, amekanusha habari kuwa amekuwa hawajali wazazi wake baada ya taarifa hizo za chini chini kuzagaa na kufika kwa mwenyewe.
Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Wolper alisema kuna mengi amekuwa akiyasikia dhidi yake yakiwamo ya kutowathamini wala kuwajali wazazi wake, akisema huo ni uzushi mtupu unaolenga kumchafulia heshima yake mbele ya jamii.
Alisema kuwa wazazi wake hawana shida na msaada wake kwani hata wao ni matajiri, wana pesa na kwamba hawahitaji fedha kutoka kwake.

“Kwa pesa gani nyingi nilizonazo za kuwafikia wao hadi kuwapa matunzo? Kwani mimi bado nipo mikononi mwao na ninawategemea wao, wazazi wangu ni matajiri sana, hivyo wanaodai nimetelekeza wazazi ni waongo tu,” alisema.
Aliwataka watu hao wanaozusha habari hizo wasifanye hivyo kwani, hakuna ukweli ndani yake, yeye anawapenda wazazi wake na anawajali katika kila hali.
Wolper ni kati ya wasanii ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya muziki huo kutokana na ubora wa kazi alizonazo na uwezo wake wa kukaa katika kamera.
chanzo:tz daima

No comments:

Post a Comment