Tuesday, 8 July 2014

Hivi ni kwa nini? Uchumba huonekana ni dhahiri, baada na ndoa ni shubiri.

Lakini inapotokea mke anaacha kumtii mumewe na kumfanyia visa visivyofaa, wala kumjali hata awapo mgonjwa, huyu ni mwanamke wa aina gani?

Yupo mama mmoja nimesimuliwa habari zake aliyepigania sana afunge ndoa na mpenzi wake ambaye tayari walishabahatika kuzaa watoto watatu. Aliyekuwa na mchecheto mkubwa wa kufunga ndoa hiyo ni mwanamke kwani alikuwa radhi hata anunue pete za harusi. Alipoona kuna uchelewesho alizinunua.


Ndoa ikafungwa na baada ya mwaka mmoja tu tayari mama huyu akaanza kufungua makucha. Hana kazi ni mama wa nyumbani ila mumewe ndiye anayechakarika na kazi na ameweza hata kujenga nyumba ambayo wanaishi.

Baadhi ya visa vya mama huyu ni kama vifuatavyo. Mume anapougua hamjali na wala hampeleki hospitali jambo la kwanza ni kuwaita wazazi na ndugu zake waje waone la kufanya. 

Hata kama ameugua usiku atamwacha hadi asubuhi ndipo aite ndugu zake. Hii siyo sahihi kabisa kwani kama ni mtu wa kupona anaweza kupoteza maisha kwa kutopata huduma ya haraka ya kitabibu.

Pili, hataki kumwandalia mumewe chakula kinachomfaa hasa wakati wa mgonjwa, ingawa fedha za matumizi anampa zaidi ya laki mbili kwa mwezi.

 Atamdhikahi na zaidi anaweza kumpikia ugali mgumu wakati mgonjwa angehitaji chakula chepesi anachoweza kumeza haraka hasa kutokana na ugonjwa kumuumiza mdomoni.

Mwanamke huyu hana muda wa kukaa na watoto mara nyingi anawapeleka kwa ndugu zake huku yeye akibaki nyumbani akizurura kwa mashoga zake na kiguu na njia kwenye mipasho ya taarabu.

Na zaidi sana anafahamika hodari kwa kwenda kwa waganga kuvuruga matendo yake yasijulikane, huku akisahahu kuwa Mungu anaona matendo yake yote maovu anamsubiri kumwadhibu wakati atakapochagua mwenyewe. 

Hata ugonjwa wa mumewe unaaminika kuchangiwa na nyendo zake hizo za ushirikina kwani ugonjwa humpata mumewe usiku wa manane akiwa amelala. Nyumbani hausigeli hawakai humkimbia baada ya kugundua mbinu zake hizo za kuwanga usiku.
chanzo:nipashe

No comments:

Post a Comment