HITIMA ya aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Shida Salum, inatarajiwa kufanyika nyumbani kwake Tabata-Bima, Dar es Salaam Jumamosi ya wiki hii.
Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Zitto Kabwe, hitima hiyo inafanyika baada ya kutimia siku 40 tangu kufariki kwa mama yake mwanzoni mwa Juni, mwaka huu.
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), alisema kisomo cha hitima kitaanza saa 11 jioni.
Shida Salum enzi za uhai wake mbali ya kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania na Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba.
chanzo:tanzania daima
No comments:
Post a Comment