*MISS UNIVERSE 2011, KAMA SASA NDO ANA UMRI WA MIAKA 18, ALIKUWA NA UMRI GANI MWAKA 2008

MREMBO Nelly Kamwelu (18), juzi aliibuka mshindi wa mashindano ya Miss Universe Tanzania baada ya kuwashinda wenzake 18.

Katika mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip, haikuwa kazi rahisi kwa mrembo huyo kuibuka na taji hilo kwani warembo walikuwa na ushindani mkubwa.
Kutokana na ushindi huo, Nelly ambaye alishiriki Miss Tanzania mwaka 2008 na kushindwa kufanya vema, ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa yatakayofanyika Septemba nchini Brazil.

Hali ilikuwa tofauti kwa Nelly baada ya aliyekuwa jaji mkuu, Maria Sarungi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Compass Communications, inayoratibu shindano hilo, kumtangaza mshindi.
Hiyo ilitokana na ushindani mkali uliokuwepo kati yake na Neema Kilango na Yacoba Assenga ambao walikuwa tishio tokea kuanza kwa mashindano hayo.

Nelly ambaye alijikita katika urembo mwaka 2008 na kushika nafasi ya pili katika shindano Miss Ilala na Miss Dar City, alisema anashukuru kwa kuwaa taji hilo kwani pamoja na kushinda ushindani ulikuwa mkali.

Kwa ushindi huo, Nelly alijinyakulia kitita cha shilingi milioni 3 na kupata ‘schoralship’ ya kwenda kusoma nchini Marekani katika chuo cha New York Film Academy ambako atachukua kozi ya mawasiliano ya umma na utengezaji wa filamu.

Mbali na zawadi hizo pia alijinyakulia simu ya Blackberry kutoka mtandao wa Jamii Forum, tiketi tatu za ndege kwa ajili ya safari za kufanya kazi za jamii kutoka Precision Air, vipodozi vyenye thamani ya shilingi 350,000 kutoka Shear Illusion na mafunzo ya mwaka mmoja yatakayotolewa na Mercy G Beauty ambao wote ni wadhamini.

Neema Kilango alishinda nafasi ya pili na kupata sh. milioni 1 na kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Earth nchini Thailand.
Neema pia alishinda taji la Miss Congeniality na kupata ofa ya kusoma masomo ya ujasiriamali yenye thamani ya dola 1,500 za kimarekani.

Yacoba Assenga aliibuka mshindi wa tatu na kuzawadiwa sh 500,000 na kushinda nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss International.

Vile vile Linda Deus aliibuka na taji la Miss Entrepreneurial Mind set na kupata ofa ya kusoma masomo ya ujasiriamali yenye thamani ya dola 1,500 za kimarekani.

Mashindano ya Miss Universe yalifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2007 ambapo Flaviana Matata aliibuka mshindi sambamba na kufanya vyema katika mashindano ya kimataifa yaliyofanyika nchini Mexico.

Flaviana ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani, aliingia hatua ya 10 bora (nusu fainali) na baadaye Amanda Ole Sulul aliiwakilisha Tanzania mwaka uliofuata na kufuatiwa na Illuminata James na mwaka jana Hellen Dausen.

Nelly Kamwelu wakati akiwa amepatwa na mkasa huo alikuwa ni Miss Ilala mwaka 2008. 
Kidogo ilivyokuwa wakati wa kesi (...........Wakili wa serikali, Misonge, alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mirumbe kuwa mnamo Machi 14 mwaka huo majira ya saa tano usiku eneo la Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.............) 

KILA LA KHERI DADA NELLY!!!!!!