Wednesday, 22 June 2011

LINA KUGEUKIA BONGO MOVIE?

MSANII wa muziki wa kizazi kipya katika miondoko ya zouk, Esterlinah Sanga ‘Linah’, hivi karibuni alipewa ushauri wa bure wa kugeukia utengenezeji wa nyimbo zake filamu.
Ushauri huo alipewa na mtangazaji wa kituo cha Star tv, Sauda Mwilima katika mahojiano baina yao katika kipindi chake cha mcheza kwao.
Linah ambaye katika mahojiano hayo alisema baada ya kutoka na nyimbo ya atatamani, bora nikimbie na lonely, siku za karibuni anatarajia kuachi kitu kipya kitakachokwenda kwa jina la ‘Nimetulia’, zote zikihusu mikasa ya mapenzi.
Kwa hali hiyo, Mwilima alimweleza Linah anaonaje kama nyimbo hizo akazitengenezea filamu, kama ilivyokuwa kwa Twenty Parcenty kwa kuwa mashairi yake tu ni script tosha, pia atajiongezea kipato.

No comments:

Post a Comment