Wednesday, 22 June 2011

Muhogo Mchungu: Fedha ya maigizo kiduchu mno !!!!!!!!

MSANII wa maigizo, Abdallah Mkumbira ‘Muhogo Mchungu’,amesema kitendo cha wengi kuigiza, kumeshusha hadhi ya fani hiyo.
Muhogo Mchungu alisema igizo moja linaloruka katika kituo cha televisheni, hulipwa shilingi 300,000, fedha ambayo ni ndogo ukilinganishwa na gharama za kuandaa mchezo mzima.
Kwa mazingira hayo, amewataka wamiliki wa vituo vya televisheni kubadilika na kujali thamani ya kazi za wasanii.
Akizungumzia kuhusu tasnia ya filamu kwa sasa, Muhogo alisema inaenda vizuri na  kutoa angalizo kuwa, ni vema wasanii wakarudi kwenye uhalisia wa maisha ya Mtanzania.

No comments:

Post a Comment