Mashabiki wa timu DC Motema Pembe imemdhalilisha Mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la JamboLeo, Asha Kigundula wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Simba na DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Jumapili iliyopita.
Mwandishi huyo pamoja na Watanzania wengine waliokuwa Kinshasa, DRC kushuhudia mchezo wa Simba na DC Motema Pembe kwenye Uwanja wa Mashujaa ‘Stade des Martyrs’ walifanyiwa fujo ambazo hatukutarajia kama mashabiki wenye busara wangeweza kuzifanya.
Cha kusikitisha zaidi ni hatua ya mashabiki hao kumdhalilisha mwandishi huyo bila kujali utu wake, heshima yake na thamani yake, kisa tu ni Mtanzania ambaye alikuwa uwanjani hapo kushuhudia timu ya Tanzania ikicheza.
Habari zilizotolewa na watu walioshuhudia mkasa huo walisema kwamba, mwandishi huyo alikuwa anatakwenda msalani na ndipo mashabiki hao walipoanza kumzonga na ghafla akatokea mtu mmoja akajifanya msamalia kumbe muongo, akampeleka hadi msalani lakini kilichofuata walipofika huko, akaamuriwa ajisaidie bila kufunga mlango halafu akapekuliwa kila mahali mwilini mwake na kuvuliwa flana alovaa ambayo ilikuwa ni jezi ya Simba FS.
CHAMA Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimesikitishwa na kinalaani tukio.
No comments:
Post a Comment