MUIGIZAJI wa vichekesho, Twahir Shabani ‘Mjaluo’ au ‘Rais wa wacheza viduku’, ametoboa siri kuwa aliyemvutia kuingia katika tasnia hii ya uigizaji wa vichekesho ni mwigizaji wa vitimbi wa nchini Kenya anayejulikana kwa jina la Mzee Ojwang.
kuwa muigizaji huyo alikuwa akimfuatilia tangu mdogo, na kila kipindi chao kilipokuwa kikimalizika naye huanza kuongea kama mzee huyo, na kadiri siku zilivyozidi kwenda akajikuta uigizaji wake unakuwa na hatimaye kuweza kuongea kama yeye.
Hata hivyo Mjaluo ambaye jina lake lilianza kukua kupitia mashindano ya kutafuta wachekeshaji katika kituo cha Eatv, na kubahatika kuingia kumi bora, likuwa akiigiza kama mlevi, lakini kutokana na sasa kufanya kazi katika Kampuni ya Al-rihamy, anasema alilazimika kubadili uigizaji huo ili asifanane na muigizaji Masele ambaye wapo naye.
Kuhusu kutoa filamu ya kawaida ama ya vichekesho mwenyewe Mjaluo anasema bado hajafikiria hilo kwa sasa, kwani lengo lake ni kuja na kitu tofauti, hivyo bado anajifunza kutoka kwa wasanii wengine.
No comments:
Post a Comment