MKAZI wa Mbezi Juu, Magdalena Sebastian, anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 25, amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kanga.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi, majira ya saa 2 usiku na mwili wa marehemu ulikutwa ukining’inia kwenye kenchi.
Kwa mujibu wa maelezo ya baba yake mdogo, Jonas Sebastian, Magdalena alikuwa akisumbuliwa na ugojwa wa Ukimwi. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
Katika tukio jingine, mtembea kwa miguu, Yusuph Mohamed, ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Gongo la Mboto, amefariki dunia baada ya kugongwa na gari.
Ajali hiyo ilitokea juzi, majira ya saa 2 asubuhi wakati gari aina ya DCM lililokuwa likiendeshwa na dereva asiyefahamika akitokea Mombasa kuelekea Gongo la Mboto kumgonga Mohamed. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Kisarawe.
No comments:
Post a Comment