Friday 15 July 2011

" UJIO" AMEAMUA KWENDA DARASANI (UDSM) KUSOMEA FANI YA SANAA

MSANII wa maigizo, Netho Nazareti  ‘Ujio’, ameamua kwenda darasani ambapo sasa hivi yupo mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akisomea fani ya sanaa.
 Ujio ambaye jina lake lilitamba katika kundi la Kaole, akiigiza kama zezeta, alisema ameamua kwenda darasani baada ya kuona kuwa kufanya fani ya sanaa bila elimu ni kazi bure.
Ujio anasema baada ya kwenda shule ameweza kupata uelewa mpana kuhusu fani nzima ya sanaa na kuongeza kuwa, kwa sasa uigizaji wa wasanii wengi hapa nchini ni wa ku – ‘copy’ na ku – ‘paste’.
 “Kwa mfano katika suala la mavazi, mtu anachoigiza ni tofauti na kile anachokivaa, lakini huku chuo tunafundishwa jinsi gani unatakiwa uende sambamba na vitu hivyo,” anasema.
Matarajio yake baada ya kumaliza chuo, anasema ni kufungua studio yake ya kutengeneza filamu, ambayo anadai kutokana na kupikwa chuoni kuhusiana na suala zima la utengezaji wa filamu, itakuwa tishio kwa studio zingine.

No comments:

Post a Comment