Saturday 16 July 2011

MUSA KITALE ANATARAJIA KUACHIA FILAMU "MORE THAN LION"

MSANII wa vichekesho na maigizo, Musa Kitale, aliye maarufu kwa jina la Kitale, hivi karibuni anatarajia kuachia filamu yake mpya itakayokwenda kwa jina la ‘More than a Lion’ ambapo ndani yake amemshirikisha msanii wa muziki wa kizazi kipya, Dogo Janja wa kundi la Tip Top Connection.
Kitale alisema katika filamu hiyo ambayo amecheza kama mhusika mkuu, anaonekana kuwa mkali sana kwa wadogo zake, mpaka anajikuta anaharibu.
Katika filamu hiyo ambayo alisema ipo katika hatua za mwisho kuihariri, amewashirikisha pia wasanii wengine aliocheza nao katika tamthilia ya Jumbo la Dhahabu kama vile Mzee Kaangaa, Kisosi na Aunt Kame.
Hata hivyo Sayari ilipomdodosa ili kujua kama alishawahi kutumia mihadarati kidogo kutokana na michezo mingi kupenda kuigiza kama teja, Kitale alisema hajawahi na wala hatumii kilevi cha aina yoyote.

No comments:

Post a Comment