Tuesday, 5 July 2011

VICHEKESHO WANAVYOVIANDAA SASA HAWAITAJI WANAWAKE WENYE MAUMBILE MAKUBWA(KING MAJUTO)!!!!!!!!


mkonge wa vichekesho amesema kuwa vichekesho wanavyoviandaa kwa sasa hawahitaji wanawake wenye maumbile makubwa...
King Majuto!
Baada ya kutamba na filamu ya Inye ambayo ilijipatia umaarufu kutokana na wanawake wengi wenye makalio makubwa walioshirikishwa kwenye filamu hiyo, King Majuto amesema kuwa katika filamu zao za sasa hawahitaji tena wanawake wenye makalio makubwa.

King majuto alisema kuwa wanawake wenye maumbile makubwa waliwahitaji
kwenye vichekesho vya Inywe tu ili kufikisha ujunbe kwa wanawake kama
wale wanaovaa nguo ndogo ili kuwatamanisha wanaume.

"Tulifanya vile ili kufikisha ujumbe tu lakini kwa ujinga wa watu wanabaki kucheka tu bila kuangalia ujumbe uko wapi, wenyewe wanasema tumewadhalilisha lakini si kweli sisi tunataka waache kuvaa nguo za kubana tu," alisema King Majuto.

Alisema kuwa watu wengi wanadhani vichekesho ni kucheka tu hivyo ni
vizuri kumlenga mtu moja kwa moja ili mwenyewe ajue ili aache kabisa
tabia ambazo hazifai.

Aidha King huyo wa vichekesho amedai kuwa mkataba alioungia na Al-Riyami unambana kuwaonesha wapenzi wake makeke yake upande wa filamu.

"Nimeandaa filamu zangu mkataba ukiisha tu wale wanaojiita masupa staa
katika filamu wakae pembeni kwa sababu mimi ni mkali kuliko wao nitawakimbiza tu," alisema King Majuto



No comments:

Post a Comment