Tuesday, 5 July 2011

APEWA KIFUNGO CHA NYUMBANI!!!!!!

Aliyekuwa mkuu wa shirika la fedha duniani, IMF Dominique Strauss-Khan ameachiwa huru baada ya kupewa kifungo cha nyumbani na kurejeshewa dhamana yake ya dola za kimarekani milioni 3.7.

Imeripotiwa na waendesha mashtaka wamekubaliana kuwa Bw Strauss-Khan aachiliwe huru "kwa udhamini wake mwenyewe," ikimaanisha aahidi kufika mahakamani.

Anatuhumiwa kumdhalilisha kijinsia mhudumu kwenye hoteli moja mjini New York mwezi Mei 14.
Lakini kesi hiyo inakaribia kufutwa baada ya kuibuka mashaka makubwa juu ya uaminifu wa aliyemshtaki.

Mwanasiasa huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 62 - aliyeonekana kuwa miongoni mwa wagombea wa urais wanaoongoza- alifika mahakamani siku ya Ijumaa.

Baada ya kutathmini taarifa za mwendesha mashtaka kutoka kwenye ofisi ya mahakama ya wilaya ya Manhattan, jaji ametangua masharti makali ya dhamana aliyopewa na Bw Staruss-Khan, lakini aliamuru kushikiliwa kwa hati yake ya kusafiria ili asiweze kusafiri nje ya Marekani.

Miongoni mwa yaliyowasilishwa ni taarifa kuwa mhudumu huyo alitoa ushahidi usio wa kweli kwa wazee wa baraza, bila kusema alisafisha chumba chengine kabla ya kumwambia msimamizi wake juu ya madai ya kudhalilishwa kijinsia.

No comments:

Post a Comment