Thursday, 15 December 2011

UWOYA: BIFU LANGU NA WOLPER BADO SANA


MWIGIZAJI anayetamba katika Bongo Movie, Irene Uwoya amesema bifu lake na mwigizaji mwenzake, Jaquline Wolper, halitaisha.
Alisema hali hiyo inatokana na jinsi ambavyo alimdhalilisha, akimzushia kumchukulia mchumba wake, wakati yeye ana mume wake wa ndoa.
“Mimi siwezi kumsamehe Wolper, kwanza ni mshamba na anataka ustaa kwa haraka na watu wasiseme, mimi nafanana nae? Si kweli, sina matendo kama yake ya kinafiki,” alisema Uwoya juzi katika kipindi cha Take One cha Clouds TV.
Aidha, Uwoya amewataka wasichana wanaoshiriki uigizaji kujituma na kuacha kutumia nafasi hiyo vibaya kwa lengo la kutaka kupata umaarufu tu kupitia televisheni au kuuza sura.
Uwoya alisema wasichana wengi wameingia katika fani hiyo kujitafutia umaarufu tu, wakisahau kuonesha uwezo na vipaji vyao halisi.
“Wanadada wameona kuwa maigizo ni sehemu ya kuwa staa na kuuzia sura, hivyo wanashindwa kujua na kufanya kitu kilichowaleta katika tasnia hii ya uigizaji,”alisema.
Uwoya alisema wasichana wamekuwa wakiitumia vibaya fani hiyo kwani mbali ya kuuza sura, pia wamekuwa wakifanya matendo ya ajabu kiasi cha kuitia doa tasnia hiyo yenye heshina na dhima muhimu kwa jamii.
“Siku hizi wasichana wanatumika vibaya, mtu anaweza akaja na kukwambia mfano Uwoya unaitwa na mtu fulani ana laki moja, na wasichana hao wanakwenda na kuchukua hizo fedha kwa kuuza miili yao, ila kwangu mimi mtu hawezi kuja na kuniambia upuuzi kama huo,” alisema Uwoya.

No comments:

Post a Comment