Thursday, 29 December 2011

WEMA LULU KUTOKA PAMOJA!

MSANII Suleiman Said (Barafu) anatarajia kuachia filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Houseboy’ Januari mwakani, huku wasanii Wema Sepetu na Elizabeth Michael ‘Lulu’ wakiibeba wakiwa miongoni mwa wahusika wakuu. 
 Barafu alisema tayari filamu hiyo ipo katika hatua za mwisho za kuimalizia na ifikapo Januari, mashabiki wategemee mambo mazuri kwa kuwa imebeba mambo mengi ya kujifunza. 
Akidokeza kwa kifupi kilichochezwa katika movie hii, Barafu anasema kuna shambaboy mmoja aliingia katika familia ya watu na kujikuta akiwapachika mimba; mama, mtoto na dada yake ambapo baadaye anatoboa siri iliyomfanya kutenda kosa hilo la kidhalimu.

No comments:

Post a Comment