NILIKUWA miongoni mwa Watanzania walioshuhudia kuwekwa jiwe la msingi la kiwanda kikubwa barani Afrika cha saruji mkoani Mtwara.
Niliona namna viongozi wa serikali walivyokuwa wamejawa na tabasamu na bashasha tele, wakiongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati wote wa shamrashamra za sherehe hizo.
Kwa masikio yangu, nikapokea sauti iliyojaa matumaini na furaha ya Waziri Mkuu Pinda, akimpongeza mfanyabiashara nguli wa Nigeria, Aliko Nangote, kwa uamuzi wake wa kuja kujenga kiwanda kikubwa, kizuri na kitakachoajiri na kuleta neema katika mikoa ya Mtwara na Lindi.
Bado nakumbuka namna Nangote alivyoenziwa na serikali siku hiyo. Sitaki kukumbuka maneno mengine ya kukatisha tamaa yaliyotolewa na baadhi ya wananchi. Moja, tu ni kwamba tukio hilo, lilitokea katika kipindi ambacho Mtwara uligubikwa na wimbi la vurugu kubwa zilizosababisha maafa kwa maisha ya watu na mali katika sakata la gesi.
Serikali siku hiyo ilikuwa ikifurahia uwekezaji wa raia wa kigeni, Mwafrika ambaye historia inabainisha kuwa mafanikio yake yalichangiwa vema na sera za nchi yake.
Waziri Mkuu alikuwa akifurahia uwekezaji wa Mwafrika mwenzetu huyo, ambaye alisaidiwa kufika hapo alipo si kwa vijembe, roho mbaya na vigingi vya watawala wa taifa lake, bali msaada wa watawala na mifumo sahihi ya kibenki ya Nigeria iliyolenga kuwasaidia wajasiriamali wazawa kufanikisha malengo yao.
Ninacheka kwa uchungu, Watanzania wanapowaona viongozi wao wa serikali waliowachagua kwa kuamini kuwa watawasaidia na kuwaongoza kufikia Tanzania isiyo na umaskini, wakiwa tayari kufanya lolote na kutoa chochote kuwasaidia wawekezaji wa nje, na wakati huo huo ikiwapiga teke la mbavu watu wake.
Watanzania wenye akili zinazofanya kazi ya kuchambua na kunyumbulisha mambo muhimu ya nchi, bado wanayo kumbukumbu iliyojaa uchungu wa shubiri ya namna watu kutoka nje ya nchi, walivyokuja nchini wakinuka vikwapa, kwa umaskini, lakini miaka miwili baadaye wakaondoka wakiwa matajiri wa kutupwa.
Miaka ya tisini kuna raia mmoja aliingia nchini akiwa hana hata senti ya uwekezaji. Akabebwa na watawala, akasifiwa kwa kila neno, na kisha akachota kiasi kikubwa cha fedha benki huku akinadiwa kwa sifa za mfanyabiashara maarufu.
Wanaokumbuka jambo hili wanajua namna mtu huyo alivyotoroka nchini baadaye akituacha midomo wazi. Majitapo na majigambo ya watawala kwamba anasakwa, yamekuwa kama wimbo wa watoto wanaobembelezana bila msaada.
Hilo halikuwa fundisho kwa serikali ya wakati huo na nyingine zilizofuata. Bado tunakumbuka miaka miwili tu kama si mitatu iliyopita, kiongozi mmoja wa Umoja wa Vijana wa CCM alivyocharuka akipinga ujenzi wa jengo kubwa katika kiwanja kinachomilikiwa na umoja huo.
Kada huyo ambaye sasa hasikiki tena akipinga baada ya kupewa ulaji, alikaririwa akisema wazi kuwa, aliyekabidhiwa uwanja huo akidaiwa kuwa mwekezaji hakuwa na pesa yoyote, badala yake alitumia hatu ya umiliki wa jengo la kihistoria la UVCCM kwenda kukopa fedha benki kujenga jengo hilo.
Serikali, CCM, UVCCM wala huyo mwekezaji hawakuwahi kukanusha tuhuma hizo, na jengo limekamilika na mtu anakula pesa yake taratibu!
Achukie nini sasa, ama alalamike nini ikiwa wenye nchi wamemruhusu? Tumlaumu kwa lipi zaidi tu ya sisi wanyonge kuachia kicheko cha uchungu?
Basi kwa huruma hiyo hiyo, serikali ingewatendea hivyo hivyo wawekezaji wa kizalendo wenye nia na moyo wa kujenga nchi yao. Badala yake, tumeshuhudia na tunaendelea kuona kwa macho yetu, watendaji wa dola wanavyowasukumia mbali wazalendo wanaowania kufikia mafanikio halali kama ya Dangote wa Nigeria.
Mtanzania mwenzetu na mzalendo wa kweli, Reginard Mengi, hana tofauti yoyote na Dangote aliyefanikiwa kufikia kiwango cha kuja nchini na kufanya kile ambacho serikali huru iliyojitawala kwa miaka 50 imeshindwa kukifanya.
Mzee Mengi ambaye wengi wetu tunajua namna alivyopambana kwa akili, juhudi, maarifa na nidhamu ya hali ya juu kufikia mafanikio aliyonayo, amejitosa mara kadhaa kutaka kuinua uchumi wa taifa kwa kuwekeza katika miradi kadhaa.
Alijaribu katika sekta ya huduma za kitalii akitaka kuwekeza katika mahoteli yaliyokuwa yakisuasua katika uendeshaji, lakini akatimuliwa vumbi na wale wale wanaopiga panda kila siku kualika wawekezaji wenye nia na moyo.
Reginald Mengi, pamoja na baadhi ya wafanyabiashara, amejaribu safari hii kusimama na kuitaka serikali kuwaunga mkono wawekezaji wa ndani kwa hali na mali ili waweze kuendesha shughuli za mradi wa gesi kwa manufaa ya taifa.
Katika hali yoyote ile, na kwa uungwana wa hali ya juu na uliolenga kuinua uchumi wa Watanzania ambao watawekeza hapa hapa na faida yake kubaki hapahapa nchini, ilitegemewa serikali kumuunga mkono mzee Mengi na wengine katika nia thabiti ya kuwekeza.
Badala yake, Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, bila wasiwasi, ndani ya suti yake ametamka bila kupepesa macho kuwa Watanzania hawana uwezo wa kifedha kuwekeza katika utafiti wa gesi na mafuta, zaidi ya kuwa na ujuzi na mtaji wa kuuza juisi!
Hivi mtu unaposikia kauli mbaya kama hii anaambiwa mfanyabiashara aina ya Mengi na wengineo kama yeye ikitoka katika kinywa cha mtu mwenye hadhi ya uwaziri, unafanya nini zaidi ya kucheka kwa uchungu tu?
Kama serikali iliwawezesha wachuuzi wa kigeni kupata fedha kutoka katika benki zetu, nongwa inatoka wapi kufanya hivyo hivyo kwa Raginald Mengi na wenzake? Kwanza huyu ni Mtanzania, atajenga na kuajiri Watanzania wenzake. Atajenga majumba kwao Uchagaji, na kwingineko. Hivi kipi bora kumpa ngozi nyeupe ambaye ataondoka na kujenga kwao?
Leo mzee Mengi anasimangwa kama mtoto, wakati ni huyu huyu aliyebuni na kusaidia nchi wakati ilipokabiliwa na ukosefu wa bidhaa muhimu kama sabuni za kuogea, dawa za miswaki , rangi za viatu na hata kalamu?
Ni mzee Mengi ambaye hana taaluma ya uandishi wa habari, lakini leo hii ndiye kinara wa vyombo vya habari hapa nchini kuliko hata serikali yenyewe!
Kama ametumia hiyo faida yake ya kuuza juisi kuanzisha magazeti, radio na runinga kiasi cha kuajiri mamia ya Watanzania, atashindwa vipi kutumia akili na maarifa hayohayo kuendesha biashara za gesi na mafuta?
Kama Mengi na wengine angalau wanazo hela za juisi, kwa maana kwamba wana viwanda vyao ndani ya Tanzania na wameajiri Watanzania, kichefuchefu kinatoka wapi, kwa serikali kuwasaidia wazawa kwa kuwachukulia dhamana ya kukopa mitaji mikubwa kama wanavyowafanyia wageni? Kisa, hawa ni Waswahili na wale ni weupe? Upofu ama kitu gani?
Kwamba badala ya kuwakuwawezesha serikali imewageuka na kuwasimanga na kuwabeza kuwa hawana uwezo wa kifedha kuwawezesha kushiriki katika michakato ya kupewa vitalu vya utafiti wa gesi na mafuta, badala yake inakimbiza fursa hiyo kwa wageni.
Hawa weupe wanaotetewa na Waziri Muhongo, sasa tunaambiwa hakuja na senti. Kwamba alichofanya ametumia leseni ya kampuni yake kama dhamana katika moja ya benki za hapa nchini ili apewe mkopo!
Hivi mzee Mengi na Watanzania wengine hawana leseni? Hii ya Mzungu kapewa mbinguni? Ni ya rangi gani? Watanzania tunapoifikiria serikali yetu katika mambo kama haya tunaishia kucheka kwa
chanzo:daima
No comments:
Post a Comment