WAKATI Tanzania Bara filamu za kibongo zikiwa zimetapakaa kila kona, kwa upande wa Tanzania Visiwani kuzipata ni ishu.
Mwandishi wa habari hizi alizunguka takribani maduka yote ya visiwani humo, kuulizia filamu hizo na kuambiwa hakuna.
Alizikuta katika duka moja tu lililopo mitaa ya soko la Darajani.
Hata hivyo baadhi ya wakazi waliohojiwa walisema filamu hizo zimekuwa zikikosa soko kutokana na mavazi ambayo waigizaji wamekuwa wakiyavaa ambayo hayaendani na maadili ya Wazanzibar.
Kwa upande wa wauzaji, walisema wanapouza filamu hizo hawapati faida zaidi ya kupewa, jambo ambalo linawawia vigumu kufanya kazi na wasambazaji wa filamu hizo ukizingatia kwamba kuna filamu za kizungu ambazo wakiuza faida yao wanaiona hapohapo.
No comments:
Post a Comment