Gwambo anayefanya mafunzo kwa vitendo katika hospitali ya Serikali ambayo haikutajwa mahakamani hapo, jana alisomewa mashitaka mbele ya Hakimu Benedicta Beda.
Mwendesha Mashitaka Masini Mussa, alidai kuwa kati ya Machi 24 mwaka jana na Aprili 2 mwaka huu eneo la Manzese, Gwambo alimwingilia kinyume cha maumbile mtoto huyo.
Aliendelea kudai katika mashitaka ya pili kuwa kabla ya kumlawiti, Gwambo alimpiga mtoto huyo na kumsababishia maumivu na majeraha mwilini.
Mshitakiwa alikana mashitaka na kurudishwa rumande hadi Mei 8 kesi hiyo itakapotajwa.
Wakati huo huo, mkazi wa Kibamba katika Manispaa ya Kinondoni, Mustafa Wachega (39) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na mashitaka ya kumnajisi mtoto wa kaka yake. Wachega alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi, Athuman Nyamlani.
Mwendesha Mashitaka, Magoma Mtani alidai kuwa Aprili 17 eneo la Manzese Tip Top, Wachega alimwingilia kimwili mtoto huyo wa kike mwenye umri wa miaka 16 anayedaiwa kuwa ni wa kaka yake. Mshitakiwa alikana mashitaka na kuachiwa kwa dhamana baada ya kukidhi masharti ya dhamana, kesi yake itatajwa Mei 8.
chanzo na habari leo
No comments:
Post a Comment