Thursday, 6 June 2013

Hadithi,Hadithi...........Hadithi njoooo utamu kolea HAPO ZAMANI ZA KALE........BINADAMU HANA WEMA

Hapo zama za kale palikuwa na kijana mmoja aliyekuwa akijulikana kwa jina la Sande akiwa anaishi na mama yake.

Siku moja sande akamwambia mama yake kuwa anataka kwanda kuishi mbali akiwa peke yake.
Lakini mama yake akumwambia kwa nini mwanangu unaatka kuishi mbali mimi nibaki peke yangu?

Sande akamwambia mama yake kuwa anataka akakae mbali na watu.
Sande akaamua kuondoka akamwacha mama yake, mkononi akiwa amebeba panga na kamba.

Akatembea umbali mrefu mpaka akafika kwenye msitu mkuuuubwa sana. Kwenye huo msitu akaona shimo kubwa sana. Alipoangalia ndani ya lile shimo akamuona binadamu, simba, nyoka na nyani.
Wale viumbe wakamlilia sana Sande awato mle shimoni na hatimaye Sande akapatwa na huruma akachukua kamba akarusha shimo na kuanza kuwaokoa.

Aliporusha kamba mara ya kwanza, nyani akaidaka akamvuta akatoka. Nyani alipofika juu akamwambia Sande, " Nakushukuru sana kwa kuniokoa umeyanusuru maisha yangu ila nakuomba umuokoe simba, usimuokoe binadamu kwa sababu binadamu hana wema".

Akarusha kamba kwa mara ya pili akadaka simba akamvuta akatoka, alipofika juu akamwambia Sande " Nakushukuru sana kwa kuniokoa umeyanusuru maisha yangu ila nakuomba umuokoe nyoka, binadamu muache kwa kuw binadamu hana wema."

Aliporusha mara ya tatu akadaka nyoka, akamvuta mpaka juu akatoka, alipofika juu akamwambia Sande "Nakushukuru sana kwa kunioko, umeyanusuru maisha yangu lakini nakuomba ondoka zako, usimtoe binadamu kwa sababu binadamu hana wema."

Sande akamwambia sawa nimekusikia, yule binadamu kule chini kwenye shimo alilia sana kwa kumuomba msaada Sande tena kwa maneno mengi. Yaani wewe umeamua kuwaokoa wanyama unaniacha mimi binadamu mwenzako nk.

Sande kwa huruma akarusha kamba kwenye shimo, binadamu akashika kamba akavutwa mpaka juu. Akamshukuru sana siku ile kwa kuokoa maisha yake.

Sande akaamua kujenga nyumba yake kwenye msitu ule akiishi peke yake. Mara nyingi nyani alikuwa akienda kumtembelea Sande pale nyumbani kwake huku akiwa amebeba mihogo, mahindi, ndizi na vyakula vingi ambavyo aliweza kuiba kwenye mashamba ya watu ili rafiki yake asipate njaa.

Simba naye alikuwa akienda kumtembelea mara kwa mara na tena kumuwekea ulinzi ili asiweze kudhuliwa na wanyama wengine. Simba alikuwa anamuonea huruma sana rafiki yake huyo kwa kuishi kwa upweke pale msituni, siku moja akapita kwenye mitaa akamukuta binti wa mfalme akamdaka akampeleka mpaka kwa rafiki yake Sande. 

Akamwambia "Rafiki yangu nimekuona upo mpweke sana hapa nyumbani kwako, hakuna mtu wa kukusaidia kazi kama vile kupika, sasa nimekuletea huyu msichana uishi naye" Sande akamshukuru sana simba kwa kumjali.

Huko nyuma lamgambo likalia kwa Mfalme, wakatangaza kwamba binti wa mfalme amepote hivyo anatakiwa atafutwe haraka iwezekanavyo.

               USIKOSE KUSOMA INAENDELEA TOLEO LA PILI

No comments:

Post a Comment