Friday, 20 April 2012

MAMA KANUMBA SASA AULAAAA!!!!


MEELEZWA, baada ya watu kadhaa kushikwa wakiwa wanasambaza kazi zinazohusiana na msiba wa Steven Kanumba, wamekubali yaishe ambapo sasa faida watakayoipata watagawana na mama mzazi wa msanii huyo.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifamba, aliiambia Sayari kuwa, baada ya kamatakamata waliyoifanya wiki iliyopita, wengine waliamua kujisalimisha.
“Hadi sasa, wafanyabiashara wengi wa kazi za Kanumba wameshaanza mazungumzo na familia ya marehemu, wamefikia mahali pazuri, na bado tunaendelea na msako kote nchini,” alisema.


           CHAZO CHA HABARI NA GAZETI LA SAYARI

No comments:

Post a Comment