MWIMBAJI wa kundi la T-Moto, Jokha Kassim ameweka wazi kuwa kwa sasa anajuta kuachana na Mkurugenzi wa Jahazi Modern, Mzee Yussuf ‘Mfalme’.
Jokha alibainisha hayo Jumamosi iliyopita alipokuwa akihojiwa na runinga ya ITV, katika kipindi cha Shamsham za Pwani.
“Kiukweli, najuta sana kutokana na kuwa nimezaa naye mtoto mmoja, ambaye kuachana kwetu na kuwa mbalimbali, kutamyumbisha zaidi mtoto wetu,” alisema Jokha.
Hata hivyo, Jokha alifafanua kuwa, ukiondoa suala hilo la kumyumbisha mtoto wao huyo ambaye ni wa kiume anayeitwa Yussuf, hajuti kwa sababu ya kimapenzi.
HABARI NA GAZETI LA SAYARI
No comments:
Post a Comment