Friday 4 May 2012

BIN LADEN HAKUPENDEZWA NA JIHAD!!!


Nyaraka mbalimbali zilzochukuliwa kutoka katika nyumba aliyokuwa akiishi Osama bin Laden nchini Pakistan zimetolewa hadharani nchini Marekani, ikiwa ni mwaka mmoja tokea kuuawa kwa Kiongozi huyo wa Al Qaeda.
Nyaraka hizo zimechapishwa kwenye mtandao na kitengo cha utafiti katika chuo cha kijeshi cha West Point, nchini Marekani.
Maelezo na nyaraka 17 zilizotolewa wazi kwa umma ni pamoja na barua na mawasiliano mengineyo ya elektroniki ambayo kwa jumla ni kurasa mia moja na sabini na tano, kuanzia mwishoni mwa mwaka 2006 hadi mwezi Aprili mwaka jana, muda mfupi kabla ya Osama bin Laden kuuawa.
Watafiti wa jeshi la Marekani, ambao walishuhudia nyaraka hizo kutolewa kwa umma, wanaelezea kwamba zinaonyesha kiongozi huyo wa Al Qaeda tayari alikuwa ameanza kuudhika kutokana na muelekeo wa makundi ya Jihad.
Alikuwa anafikiria uwezekano wa muungano wa Waarabu kama jambo linalowezekana, lakini akiwashauri wafuasi wake kuangazia lengo lao la kuishambulia Marekani, na akielezea kwamba kimsingi hilo ndio lengo lao kuu.
Katika barua moja, Bin Laden anapendekeza kuangazia kuzishambulia ndege zinazomsafirisha Rais Obama katika ziara zake nchini Afghanistan, na kwamba makamu wa Rais Joe Biden atashtuka kufuatia tukio hilo na kushindwa kuiongoza nchi.
                                             chanzo cha habari bbc swahili

No comments:

Post a Comment