Saturday, 5 May 2012

FILAMU YA MAZISHI YA KANUMBA YAJA!!!


KAMPUNI ya Steps Entertaiment iliyokuwa iachie filamu ya ‘Ndoa yangu’ iliyochezwa na Steven Kanumba, imeahirisha kufanya hivyo na badala yake itaachia filamu ya mazishi ya nguli huyo aliyefariki mwezi uliopita.
Hayo yalisemwa juzi na msemaji wa kampuni hiyo, Ignatus Kambarage, katika mahojiano maalum na Sayari.
Kambarage alisema wamelazimika kufanya hivyo, baada ya mashabiki mbalimbali wa nguli huyo katika nchi za Kongo na Ghana kuomba wafanye hivyo, na tayari wameshakubaliana na mama mzazi wa Kanumba ambaye sasa hivi ndie Mwenyekiti wa Kampuni ya Kanumba The Great.

                        chanzo cha habari na sayari

No comments:

Post a Comment