Mara ya mwisho kesi hiyo ilipofika kwa ajili ya kutajwa, Aprili 23, mwaka huu, mahakama hiyo ilifurika waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali na baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kusikiliza kesi hiyo.
Kufurika watu huko kuliwafanya askari magereza kujitahidi kuweka ulinzi pamoja na kumficha msanii huyo ili asipate usumbufu wowote, jambo lililoleta purukushani kubwa na kumbana sana Lulu, kitendo kilichomfanya kulia mahakamani wakati akiingizwa mahakamani.
Kwa sasa kesi hiyo haijaanza kusikilizwa na iko kwenye upelelezi. Lulu anatetewa na Kamishna wa Tume za Haki za Binadamu Joaquine De-Mello, mawakili wa kujitegemea Kennedy Fungamtama, Peter Kibatala na Fulgence Masawe.
Lulu anakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba ambapo anadaiwa Aprili 7, mwaka huu eneo la Sinza Vatican jijini Dar es Salaam, alimuua Kanumba.
Msanii huyo anasota rumande kwa sababu kesi ya mauaji haina dhamana.
chanzo cha habari http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=29815
No comments:
Post a Comment