YANGA imekubali yaishe! Hiyo ndio kauli ya msemaji wa klabu hiyo, Louis Sendeu kuhusu kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa watani wao wa jadi, Simba.
Mabingwa hao wa soka Afrika Mashariki na Kati, Yanga, juzi walikubali kichapo hicho katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu bara kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Akizungumza na gazeti hili jana, Ofisa Habari wa Yanga, Sendeu alisema wamekubali matokeo ya kufungwa mabao 5-0 dhidi ya hasimu wao na sasa wanajipanga kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu.
Sendeu alisema kuwa kila mtu ameona kilichotokea jana na kwamba klabu hiyo kwa sasa ni kama iko kwenye matanga ikiomboleza kipigo hicho.
Wakati Sendeu akitoa kauli hiyo baadhi ya wanachama wa Yanga wamekuja juu wakitaka Mwenyekiti wa klabu hiyo Llyod Nchunga kujiuzulu.
ENDELEA KUSOMA http://www.habarileo.co.tz/michezo/?n=29858
No comments:
Post a Comment