Tuesday 19 June 2012

OBAMA NA PUTIN WAKUBALIANA KUHUSU SYRIA!



Bwana Obama amesema Marekani na Urusi zingependa kuona suluhisho la kisiasa linapatikana nchini Syria na katika kufanikisha hilo watashirikiana na pande nyingine za kimataifa kujaribu kufikia lengo hilo
Viongozi hao wawili wamejikuta kuwa na mwelekeo wa pamoja katika masuala mengi kuhusu Syria wakati wa mazungumzo yao nje ya kikao cha G20 nchini Mexico.
Viongozi hao wamejitahidi kuonyesha kuwa mkutano wao uliodumu kwa muda wa saa mbili umeimarisha uhusiano kati yao.
Rais Obama na mwenzake Putin, wamesema kuwa kuna masuala kadhaa kuhusu juhudi za kusitisha maafa nchini syria ambayo wamekubaliana kimsingi.
"Tumejadiliana kuhusu Syria na tumekubaliana kuwa lazima ghasia zisitishwe na lazima tuwe na mikakati ya kisiasa kuzuia vita vya wenyewe kwa wenyewe na maafa ambayo tumeshuhudia katika kipindi cha hivi karibuni" alisema Rais Obama.
Uhusiano kati ya Marekani na Urusi haujakuwa mzuri sana tangu Rais Putin arudi madarakani mwezi May mwaka huu.
Rais Putin hakuhudhuria mkutano wa viongozi wa mataifa tajiri duniani G8 uliofanyika mjini Washingnton nchini Marekani, na wengi walihisi kuwa alisusia mkutano huo.
Rais Obama alielezea mkutano wao kuwa wa uwazi na wakina, lakini maneno aliyotatumia yamedhihirisha kuwa pia walitofautiana.
chanzo bbc

No comments:

Post a Comment