Friday 6 July 2012

FIFA KUPIGA KURA 'Goal line technology'


Kumekuwa na shinikizo chungu nzima kwa shirikisho la FIFA kufuatia makosa kadhaa yanayohusiana na maamuzi ya mechi, ikiwemo kosa la hivi karibuni kuhusu mechi moja wakati wa michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani ulaya.
Goli lililofungwa na Ukraine dhidi ya Uingereza ilifutiliwa mbali licha ya picha za runinga kuonyesha kuwa mpira ulikuwa umevuka na kupita mstari wa goli.
Shirikisho la FIFA linatarajiwa kuidhinisha mifumo miwili, moja inayotumia kamera za video na nyingine inayotumia sensa maalum ili kubainisha ikiwa mpira Umevuka mstari wa Goli.

No comments:

Post a Comment