NAIBU Spika wa Bunge, Job Ndugai amemwadhibu Mbunge wa Kigamboni (CCM), Dk Faustine Ndungulile kutohudhuria vikao vitatu mfululizo baada ya kushindwa kuthibitisha tuhuma kwamba madiwani wa Halmashauri ya Manispaa Temeke walihongwa ili kuukubali Mradi wa Mji Mpya wa Kigamboni.
Ndugai alitumia kifungu cha 73 (3) ambacho kinampa mamlaka ya kumwadhibu mbunge aliyeshindwa kuthibitisha tuhuma alizozitoa, huku pia akiwa amekaidi kufuta kauli yake kuhusiana na tuhuma hizo.
“Kwa kutumia kifungu namba 73 cha Kanuni za Bunge, hutahudhuria vikao vya Bunge mara tatu mfululizo, askari mtoeni nje,” aliagiza Ndugai.
Awali, Dk Ndungulile alishtakiwa na madiwani wanne wa Kigamboni kwamba aliwatuhumu kupewa rushwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ili waunge mkono mradi wa kuendeleza mji huo mpya wa Kigamboni.
Madiwani hao jana waliliandikia Bunge kukanusha tuhuma zilizotolewa na Dk Ndungulile kuwa walihongwa fedha na
Profesa Tibaijuka ili kufika bungeni
Katika malalamiko yao, madiwani hao ambao walihudhuria kikao cha Bunge hapo juzi wakati Bajeti ya Makadirio ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikisomwa, walipinga madai ya Ndungulile kuwa wakazi wa Kigamboni wamemtuma na kuwa wanaupinga Mradi wa Mji Mpya wa Kigamboni.
Akisoma barua ya malalamiko ya madiwani hao iliyowasilishwa bungeni, Ndugai alinukuu maandishi katika barua hiyo yaliyosema:
“Sisi madiwani tunakanusha taarifa zilizotolewa na mbunge wetu, Faustine Ndungulile kuwa tulipewa fedha ili kuja bungeni,” inasema sehemu ya barua hiyo.
Madiwani hao waliendelea kulalamika kwamba, matamshi yaliyotolewa na mbunge huyo yamewadhalilisha na kuondoa imani ya wananchi juu yao kama viongozi, na kuwa wanamtaka aifute kauli yake na kuwaomba radhi.
Sehemu ya barua hiyo pia ilisema hakuna diwani yeyote aliyefika bungeni hapo kwa kupewa fedha na mtu yeyote, bali kwa ridhaa yao wenyewe.
ENDELEA KUSOMA HAPA:http://www.mwananchi.co.tz/habari/49-uchaguzi-mkuu/24717-mbunge-ccm-atimuliwa-bungeni
No comments:
Post a Comment