Sunday, 15 July 2012

WASTARA SASA AJIPANGA KUMRUDISHA SAJUKI INDIA

MSANII mwenye heshima tele kunako gemu la filamu Bongo, Wastara Juma amefunguka kuwa sasa anafanya kazi kwa bidii ili aweze kumrudisha mumewe Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ India kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.
Akichezesha taya na paparazi wetu, Wastara alisema baada ya Sajuki kupewa dawa ambazo anaendelea kuzitumia zilizoonesha mabadiliko ya hali yake walitakiwa kurudi tena hospitalini India mwezi wa 10, mwaka huu kwa ajili ya uchunguzi tena ili kujua kama ugonjwa umeisha au la.
Kutokana na suala hilo la kurudi tena, Wastara alisema kwa sasa amejipanga kufanya kazi kwa nguvu zake zote ikiwa ni pamoja na filamu za kushirikishwa na watu mbalimbali ili aweze kupata fedha kwa ajili ya kumsafirisha mumewe huyo kipenzi.
“Sasa hivi nimejipanga vilivyo kwani nguvu zangu zote na akili nimevielekeza kwenye kazi na Mungu anisaidie nipate fedha kwa ajili ya kurudi India. Nisingependa mume wangu aende peke yake, nitaongozana naye tena,” alisema Wastara.
chanzo:www.globalpublishers

No comments:

Post a Comment