Friday 26 October 2012

41 wauawa msikitini nchini Afghanistan

Shambulio hilo lilitekelezwa nje ya msikiti waumini walipokuwa wakishereheka siku kuu ya Eid al-Adha.
Afisaa mmoja katika mkoa huo alisema kuwa gavana wa eneo hilo pamoja na mkuu wa polisi walikuwa ndani ya smikiti huo wakati wa shambulizi.
Alisema kuwa maafisa wa serikali hawakujeruhiwa lakini polisi na wanajeshi ni miongoni mwa waliojeruhiwa.
Walioshuhudia walisema kuwa mtu huyo wa kujitolea mhanga alikaribia msikiti na kutegua mabomu aliyokuwa amefungiwa kifuani baada ya sala ya Eid kukamilika, na waumini kusimama nje ya msikiti wakijuliana hali.
Haijulikani jinsi mtu huyo alivyoweza kupita vizuizi vinne kabla ya kufikia msikiti huo. Vizuizi hivyo vya usalama viliwekwa kwa sababu watu wanahofia kushambuliwa wakati huu wa sikukuu.
Afisa mmoja wa usalama alieleza kuwa mshambuliaji huyo alikuwa amevalia sare za polisi, ambazo huenda ziliwapumbaza maafisa wa usalama katika vizuizi hivyo.
Gavana wa Mkoa, wanasiasa wa vyeo vya juu na mkuu wa polisi walikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wakishiriki sala hiyo
Shambulio hilo limetokea siku chache tu baada ya kundi la wapiganaji kuwaua maafisa kadhaa wa Serikali katika Mkoa huo, kukiwemo aliyekuwa wakati mmoja afisa mkuu wa Taliban ambaye baadaye alijiunga na Serikali katika eneo la Faryab.
Usalama umedumishwa kote nchini Afghanistan wakati huu wa siku kuu ya Eid.
chanzo:bbc

No comments:

Post a Comment