Saturday 27 October 2012

Mtetezi wa wanawake anusurika kifo DRC


Daktari Denis Mukwege alishambuliwa na watu waliokuwa na bunduki nyumbani kwake Bukavu aliko na hospitali inayowahudumia waathiriwa wa dhulma za kimapenzi.
Alihepa risasi lakini mlinzi wake aliuawa katika tukio hilo.
Daktari Mukwege ni mpasuaji mashuhuri duniani na ameshinda tuzo nyingi tu kimataifa kwa juhudi zake kutetea wanawake wanaobakwa na makundi ya waasi.
chanzo:bbc

No comments:

Post a Comment