Monday, 26 November 2012

BAHATI BUKUKU KORTINI

MWIMBAJI mahiri wa Injili Bongo, Bahati John Bukuku (pichani chini) yuko kwenye mchakato wa kutinga kortini kwa ajili ya kumburuza mumewe, Daniel Basila ili atoe talaka.
Kwa mujibu wa chanzo, Bahati ambaye wimbo wake wa Dunia Haina Huruma ameuchezea filamu, ataenda mahakamani Jumatatu ya keshokutwa lengo likiwa kuitaka sheria imsaidie aweze kupata hati ya talaka ya kutengana na mwanaume huyo ambaye haishi naye kwa miaka sita sasa.
“Bahati anasema lengo la Daniel ni kumuweka njia panda ndiyo maana aliahidi kwenda mahakamani wiki mbili zilizopita ili ashughulikie talaka lakini hakufanya hivyo, sasa Jumatatu atakwenda mwenyewe,” kilisema chanzo.
Wakati huohuo, habari zinadai kwamba Daniel amekuwa akisema wimbo wa mkewe, Dunia Haina Huruma ametungiwa yeye kama kijembe.
Risasi Jumamosi liliwasaka wote wawili kwa nyakati tofauti ili kujua ukweli wa madai hayo.
Bahati: “Mimi ninachotaka ni talaka, aliahidi mbele ya kaka yangu kwamba angeshughulikia wiki mbili zilizopita, lakini hajafanya hivyo. Kwa hiyo mimi kwenda mbele ya sheria ni sawa tu. Huo wimbo namshangaaa, kama aliwahi kufumaniwa basi kweli ni wake.”
Basila: “Nilibanwa na mambo, lakini nakumbuka ahadi, nitaitekeleza lakini naomba isiwe kwa presha sana. Kuhusu wimbo lini nimesema alinitungia mimi?”
chanzo:globalpublishers

No comments:

Post a Comment