WATU wanne wa Mtaa wa Mzinga Kata ya Kitunda wamefariki dunia na wengine wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ilala baada ya kunywa pombe aina ya gongo inayodaiwa ilikuwa na sumu.
Wakizungumza Jijini Dar es Salaam jana, mashuhuda wa tukio hilo walisema Novemba 15, mwaka huu watu hao walienda kunywa pombe hiyo saa 9 mchana kwa mama aliyetambulika kwa jina moja Rehema aliyekuwa maarufu kwa kuuza pombe hiyo. Walisema kati ya hao waliofariki alikuwa muuzaji wa pombe hiyo pamoja na anayedaiwa kuwa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) ambaye amefariki Novemba 20, mwaka huu saa 4 usiku.
Mmoja wa ndugu wa marehemu Anna Hashimu alisema Novemba 15, mwaka huu saa 9 mchana Peter Tambwe (25), aliwaaga na kuelekea kwa mama huyo kunywa pombe hiyo.
Alisema ilipofika saa 3 usiku alirudi nyumbani kwao huku akilalamika tumbo linamuuma, ilipofika saa 8 usiku alizidiwa na kupeleka kwenye Zahanati ya Kitunda wakati akitibiwa hospitalini hapo alipatwa na umauti saa 9 usiku wa kuamkia Ijumaa.
No comments:
Post a Comment