Saturday, 24 November 2012

Hii ndio ratiba ya Birthday ya Ngwasuma Msasani Club



KATIKA kuadhimisha miaka 15 tangu kuanzishwa kwake, bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ inatarajiwa kufanya onesho la aina yake kwenye ukumbi wa Msasani Club jijini Dar es Salaam Desemba 14, mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa onesho hilo, Nassib Mahinya alisema usiku huo wa aina yake, utaambatana na shamrashamra mbalimbali zilizoandaliwa ili kuwapa raha mashabiki watakaojitokeza.
Alisema, kupitia usiku huo ambao pia utawakutanisha wasanii wote waliowahi kupitia bendi hiyo tangu kuanzishwa kwake, pia itapiga nyimbo zake kuanzia zile zilizotoka kwenye albamu yao ya kwanza hadi sasa.
“Pia kutakuwa na tukio la kukata keki, sambamba na kuwapongeza wale wote waliochangia kwa namna moja ama nyingine kuifikisha hapa ilipo bendi hii,” alisema.
Mahinya aliongeza kuwa, katika kunogesha zaidi usiku huo, wasanii na makundi mbalimbali yanatarajiwa kusindikiza wakiwemo bendi ya Mapacha Watatu pamoja na wasanii wa kundi la Mtanashati Entertainment wakiwemo Dogo Janja, PNC na wengineo.
Onesho hilo limeandaliwa na Sinai Entertainment na kudhaminiwa na Mabibo Beer Wine & Spirit, Mama Mbaga Catering, Africa Media Group, Chonapi General Supplier, Benny Mlokozi Company, Big Solution, Mtanashati Entertainment, Eliado Point View, Arafa Salon, Friendship Restaurant na Masters Club.
chanzo:daima 

No comments:

Post a Comment