Monday, 19 November 2012

Watoto 5 wafariki ndani ya debe la taka


Ripoti kutoka Kusini Magharibi mwa Uchina, zinasema kuwa watoto watano wa barabarani wamepatikana wamekufa kwenye debe kubwa la taka.
Polisi wanashuku kuwa watoto hao walifariki baada ya kukosa hewa safi, baada ya kuingia kwenye debe hiyo kukimbia baridi.
Habari hizo za watoto wa kiume watano, wadogo wenye umri wa kama miaka 10, zimeshutua na kuwashangaza raia wengi wa nchi hiyo.
Matopasi walikuta miili ya watoto hao kwenye deba la taka, katika mji wa Bijie, katika jimbo la Guizhou.
Polisi wanajaribu kutafuta familia za watoto hao.
chanzo: bbc

No comments:

Post a Comment