Tuesday 11 December 2012

Barnaba ajipanga kwa albamu ya tatu


MKALI wa muziki wa kizazi kipya, Elias Barnaba ‘Barnaba’, anajipanga kufyatua albamu yake ya tatu itakayokuwa na nyimbo kumi, ikibebwa na jina la wimbo ‘Nimeona’.
Barnaba alisema jana kuwa albamu hiyo ataisambaza mwanzoni mwa mwaka ujao kwani sasa yuko katika hatua za mwisho za kuikamilisha.
Alisema katika albamu hiyo kutakuwa na nyimbo nyingi ukiwemo ‘Sorry’ ambao unafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio, ikiwa ni wiki mbili tangu uanze kusikika.
“Hadi sasa hivi nina nyimbo tano ambazo ziko tayari na naendelea kuziandaa, naomba mashabiki wangu waipokee vizuri albamu hiyo ambayo naamini itakuwa gumzo mitaani kutokana na nyimbo zilizomo ndani yake.
Mbali ya albamu hiyo, Barnaba amekuwa akiwika na albamu zake kama ‘Kilicho Changu’ na ‘Njia Panda’ ambazo zilifanya vizuri na kumweka kwenye nafasi nzuri kisanii.
chanzo:daima

No comments:

Post a Comment