Taarifa kutoka wizarani ilisema kwamba Bi Okonjo-Iweala alikuwa ametishiwa hapo awali, lakini hawakuwa na uhakika iwapo tishio hilo lilikuwa na uhusiano wowote na utekwaji nyara huo.
Nigeria ni mmojawapo wa nchi zenye visa vingi vya utekaji nyara, uhalifu unaoingiza mamilioni ya fedha kila mwaka
Siasa au fedha?
Visa vingi hutokea katika Jimbo la Delta lenye utajiri mkubwa wa mafuta, ingawaje kutekwa nyara kwa watu wakubwakubwa si kawaida.
Afisa wa usalama alisema haikujulikana iwapo sababu ilikuwa ya kisiasa au ya kifedha.
Bi Okonjo-Iweala ameongoza kampeni kubwa ya kujaribu kuangamiza ufisadi nchini Nigeria, hususan katika mpango tata wa ruzuku za mafuta.
Amechelewesha malipo kwa wanaoingiza mafuta nchini, huku akisubiri kuthibitishwa kwa ruzuku hizo.
Utekaji nyara
Lakini wadadisi wanasema kwamba utekaji nyara wenye sababu za kisisasa ni nadra sana nchini Nigeria.
Bi Okonjo-Iweala alikuwa mmojawapo wa wale waliogombea kuiongoza Benki ya Dunia katikati mwaka huu, lakini akashindwa na Jim Yong Kim
chanzo:bbc
No comments:
Post a Comment