WANAUME wawili wamefariki dunia kwa kuchomwa visu na kupigwa na mawe katika tukio la kugombea mwanamke wilayani Tarime, Mara.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya, Justus Kamugisha, alisema tukio hilo limetokea juzi kwenye eneo la gulio katika Kijiji cha Nyibaso, Tarafa ya Ingwe, wilayani Tarime.
Alisema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi, ambapo wanaume hao walikuwa wakigombania mwanamke huyo ambaye ni mjane.
Alisema katika tukio hilo, mwanamume aliyefahamika kwa jina moja la Nyamureba, mkazi wa Kijiji cha Matanka, wilayani Serengeti, alimshambulia Juma Mseti au Marwa (20), mkazi wa Kijiji cha Nyibaso kwa kumchoma na visu tumboni na kusababisha kifo chake papo hapo.
Alisema baada ya kumuua mwenzake, mwanamume huyo alikimbia, ambapo wananchi wakiongozwa na ndugu wa marehemu, walimfukuza na kufanikiwa kumkamata na kumchoma visu na kumpiga kwa mawe hadi kumuua.
Alisema kuwa mwanamke aliyekuwa anagombaniwa na wanaume hao ametoroka.
Katika tukio jingine, mwanamume mmoja anasakwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mwenzake kwa kumkata panga na kumchoma na kisu, baada ya kumwaga pombe yake.
Kamanda Kamugisha alisema jana kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 12:45 jioni katika Kitongoji cha Itandura, Kijiji cha Nyakunguru, wilayani Tarime.
Alimtaja mwanamume anayetafutwa na polisi kuwa ni Makuri Mcharo, mkazi wa kikijiji hicho na kwamba anatuhumiwa kumuua Makuri Hamisi (32) ambaye pia ni mkazi wa kijiji hicho.

chanzo:daima
No comments:
Post a Comment