Saturday, 9 March 2013

DC asononeka nyumba za watumishi kupakwa kinyesi


Mkuu wa Wilaya Kilwa, Abdallah Ulega, amekemea kitendo cha wakazi wa Kijiji cha Kinjumbi wilayani  humo, kutowapa ushirikiano watumishi wa umma na badala yake, kuwafanyia visa vikiwemo kupakaza kinyesi nyumba zao.
Kwa mujibu wa Ulega, wananchi katika kijiji hicho, pia wamekufanya hivyo katika vyumba vya  madarasa, na kubomoa kuta za mabweni ya wanafunzi wa kike.
Mkuu huyo wa wilaya, alitoa karipio hilo juzi alipokuwa akizungumza na walimu, wazazi na viongozi wa Kata ya Kinyumbi.
Alikuwa katika ziara ya kuhamasisha shughuli za maendeleo wilayani humo.
Ulega alisema kitendo cha kuendelea kuwanyima shirikiano  watumishi wa Serikali  na hasa walimu,  ni cha aibu kubwa kwa Wilaya ya Kilwa.
Alisema kama kuna migongano  baina ya wazazi na watumishi, ni vema wakaketi na kumaliza tofauti zao, ili wafanye kazi kwa ufanisi na kwa manufaa ya kijiji hicho na taifa kwa jumla.
chanzo:mwananchi

No comments:

Post a Comment