SIZYA Mkila (5), mkazi wa kijiji cha Kanyamsenga, wilayani Sikonge, Tabora, amekutwa amekufa na mabaki ya mwili wake yakionyesha kuwa ameliwa na fisi.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Diwani wa Kiloleni, Boniface Mtani, alisema mtoto huyo alifikwa na mauti alipokuwa akichunga ndama porini, Februari 15, mwaka huu.
Mtani aliongeza kuwa mtoto huyo alipatikana siku iliyofuata huku akiwa amebaki mifupa na kichwa, hali ambayo ilikuwa rahisi kumtambua na kuonyesha kifo chake kimetokana na kushambuliwa na kuliwa na mnyama.
Kutokana na tukio hilo, alisema aliitisha mkutano wa hadhara na kuwataka wananchi kuacha tabia ya kutuma watoto katika kazi ngumu ikiwemo ya kuchunga ng’ombe.
“Nimetoa wito kwa wazazi wote kwenye kata yangu waachane na tabia ya kuwatumia kwenye kazi ngumu hasa za uchungaji mifugo na badala yake wawapeleke shule……pia nimewaagiza wazazi na walezi wote kuwapeleka wanafunzi wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza kabla ya rungu la kisheria,” alisema.
chanzo:daima
No comments:
Post a Comment