Saturday, 9 March 2013

Mwili wa mwanamke aliyechinjwa wakutwa hauna kichwa wala miguu, na alichanwa kuondolewa utumbo.


MKAZI wa Kata ya Kitomanga, Tarafa ya Mchinga, Wilaya ya Lindi, Sharifa Ally (78), ameuawa kikatili baada ya kuchinjwa na watu wasiofahamika.
Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Mrakibu mwandamizi wa jeshi hilo, Leonce Rwegasira, alisema kuwa tukio hilo lilitokea Machi 2 mwaka huu, majira ya saa 8 mchana.
Alisema Sharifa alifikwa na umauti huo alipoenda shambani kwake kuchuma kisamvu na kuchimba mihogo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwake.
Rwegasira alisema mume wa marehemu, Mussa Muongo pamoja na watoto wake walikaa hadi jioni bila kumuona na kuanza kumtafuta.
Alisema alitafutwa kwa siku mbili mfululizo, na Machi 3 walipata taarifa kuwa mwili huo uligunduliwa, ukidaiwa kuliwa na mamba.
Kwa mujibu wa Rwegasira, mwili wa marehemu ulikutwa hauna kichwa wala miguu, na alichanwa kuondolewa utumbo.
Alisema Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini waliofanya unyama huo na kuwafikisha mbele ya sheria.
chanzo:daima

No comments:

Post a Comment