Wednesday, 6 March 2013
PICHA ZA ABSALOM KIBANDA:akiwa hospitali baada kuvamiwa na majambazi na kuumizwa vibaya sana.
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Habari Corporation, Absalom Kibanda, usiku wa kuamkia leo amevamiwa na watu wasiojulikana wakati akivuka geti kuingia nyumbani kwake na gari yake aina ya Nissan.
Wavamizi hao walivunja kioo cha gari lake na kumchomoa ambapo walimpiga mapanga na kumjeruhi vibaya jicho la kushoto. Baada ya kufanyiwa unyama huo Kibanda alikimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambapo amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi ‘ICU’
chanzo:globalpublishers.info
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment