Sumbawanga. Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpanda, katika Mkoa wa Katavi, imemhukumu Abisai Joseph (40) wa Mtaa wa Kigamboni, kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wake.
Hukumu hiyo kesi hiyo iliyovutia watu wengi wa mji ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Chiganga Tengwa.Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Desemba 18 mwaka jana, akiwa nyumbani kwake.
Mwendesha Mashtaka, Ally Mbwijo, aliileza mahakama kuwa siku ya tukio, Abisai alimbaka mwanaye wa umri wa miaka sita.
Alidai kuwa mshtakiwa alifanya hivyo baada ya kumvizia mtoto huyo wakati alipotoka nje kwa lengo la kujisaidia haja ndogo
Aliiambia mahakama kuwa baada ya kumaliza kumfanyia kitendo hicho cha kinyama, mtoto huyo aliingia ndani huku akilia, jambo lililoshtuma mama yake na kumuuliza mumewe, kulikoni. Mwendesha mashtaka alidai kuwa katika majibu yake, mshtakiwa alidai kuwa alimkuta mtoto nje akibakwa na mjumbe wao wa nyumba kumi
Alidai kuwa baada ya maelezo hayo, mama wa mtoto alikwenda kwa majirani kutoa taarifa na kwamba majirani walimshauri waende kutoa taarifa polisi.
Mbwijo alidai kuwa katika maelezo yake polisi mtoto huyo alikana kubakwa na mjumbe na kwamba kitendo hicho kilifanywa na baba yake mzazi Abisai Joseph
Katika kesi hiyo upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi wanne akiwemo mtoto mwenyewe aliyebakwa na mshitakiwa hakuwa na shahidi yoyote
Chanzo: mwananchi
No comments:
Post a Comment