Waziri wa Afya Zanzibar, Juma Duni Haji, ameshangazwa na wimbi la uuzaji wa dawa za nguvu za kiume uliojitokeza katika maeneo ya misikiti visiwani humu.
Akifunga mjadala kuhusu ripoti ya Kamati ya Maendelo na Ustawi wa Jamii, Wanawake na Watoto ya mwaka 2012/2013 , Duni alisema waganga wamevamia maeneo ya misikiti na kuuza dawa za kienyeji zinazodaiwa kuongeza nguvu za kiume.
Duni alisema inashangaza kuna dawa zinazouzwa na za wanaume pekee lakini akasema ni jukumu la wananchi wenyewe kuwa makini kwa vile siyo kila daktari wa tiba asilia anaweza kutibu kila aina ya maradhi.
Hata hivyo, alisema kwa upande mwingine, vyombo vya habari vimekuwa vikichangia kuwaingiza wananchi katika matumizi ya dawa ambazo hazijathibitishwa ubora wake kutokana na kutangaza bila kupata ukweli wa dawa hizo.
Alisema baadhi ya dawa zinazouzwa huchangia matatizo ya wagonjwa kutokana
na kuzitumia bila maelekezo ya kitaalam, hivyo wanapozidiwa na kwenda
hospitali, ugonjwa huwa mkubwa na wengine kupoteza maisha.
Hata hivyo, Duni alisema ataendelea kusimamia ukweli kwa vile umri wake
unafikia ukingoni.
Alisema serikali imeshatunga Sheria ya Afya ya Jamii na Mazingira namba 11
ya mwaka 2012 ambayo itasaidia kuondoa matatizo ya matumizi mabaya ya tiba
asilia.
chanzo:nipashe
chanzo:nipashe
No comments:
Post a Comment