NYOTA wa filamu nchini, Kajala Masanja aliyenusurika kwenda jela hivi karibuni, amesema anajipanga kushirikiana na wanasheria mbalimbali kuwakomboa wanawake na wasichana waliopelekwa jela kwa makosa ya kusingiziwa.
Akizungumza katika kipindi cha ‘Amplifier’ kinachorushwa na Clouds FM, Kajala alisema wakati alipokuwa mahabusu aliweza kusikiliza matatizo mbalimbali ya wanawake waliofikishwa eneo hilo bila sababu za msingi.
Watu aliowazungumzia wengi wao wanaonekana ni wasichana wa kazi za ndani ambao mabosi wao wamekuwa wakiwasingizia kuwa wamewaibia na visa vinginevyo kama hivyo.
“Mbaya zaidi unakuta bosi huyo kamtoa msichana huyo kijijini, hamlipi mshahara hata ndani ya miezi mitano na akithubutu kudai, husingiziwa kamwibia mwajiri hivyo kumfikisha polisi,” alisema.
Kajala aliachiwa huru Machi 25, mwaka huu baada ya kulipa faini ya sh milioni 13 ambayo alitakiwa kulipa au kufungwa jela miaka saba.
chanzo:daima

No comments:
Post a Comment